Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa uhusiano wa Iran na nchi jirani umeimarika kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, huku nchi hizo zikiendelea kushirikiana kwa karibu na Tehran katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza katika sehemu ya pili ya mahojiano yake ya televisheni na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka miwili tangu kuapishwa kwake kuwa Rais, Pezeshkian alisema Iran imefanikiwa kufungua na kupanua njia mpya za biashara na nchi jirani ili kupunguza athari za vikwazo vya kiuchumi vinavyoikabili nchi hiyo.
Rais huyo alieleza kuwa kiwango cha uratibu na ushirikiano kati ya Iran na mataifa jirani kwa sasa ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, jambo ambalo limechangia kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, kisiasa na kiusalama.
Aidha, aliishukuru nchi jirani kwa ushirikiano wao katika masuala ya usalama, akisema zimechukua hatua za kuzuia makundi yanayoipinga serikali ya Iran kuvuka mipaka na kuingia ndani ya nchi.
Pezeshkian alisisitiza kuwa sera ya kuimarisha uhusiano na majirani itaendelea kuwa miongoni mwa vipaumbele vya serikali yake, akieleza kuwa ushirikiano wa kikanda ni msingi muhimu wa kuimarisha uchumi, usalama na maendeleo ya Iran pamoja na eneo zima.
7 Agosti 2026 - 22:53
Msimbo wa Habari: 1849879
Rais wa Iran amesema uhusiano wa Tehran na nchi jirani umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali, huku akisisitiza kuwa ushirikiano huo umewezesha kufunguliwa kwa njia mpya za biashara ili kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi.
Maoni yako